Askofu Aomba Msamaha kwa Kumshika Mwanamuziki Kifuani Wakati Akiongoza ibada ya Mazishi


Askofu huyo aliyeongoza ibada ya mazishi ya gwiji wa muziki nchini Marekani Aretha Franklin ameomba msamaha baada ya kushutumiwa kwa kumgusa kifua mwanamuziki Ariana Grande mbele ya umati mkubwa uliohudhuria mazishi hayo.

Picha zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis akimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia upande mmoja wa kifua chake.

''Sio lengo langu kumshika mwanamke matiti'', aliambia shirika la habari la AP.

''Pengine nilivuka mpaka, pengine nilijihisi kuwa karibu naye sana kama rafiki''.

Aliongezea lakini tena naomba msamaha,  Muhubiri huyo alisema kuwa aliwakumbatia wasanii wote waume kwa wake wakati wa sherehe hiyo ya kumuaga malkia wa muziki wa soul.

Lakini waliohudhuria walianza kutuma picha kutoka katika ibada hiyo wakati Ariana aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa Aretha Franklin { You Make Me Feel a natural Woman}

Watu wengi walihisi kwamba mkono wa Askofu Ellis ulikuwa juu zaidi ya mwili wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokuwa akizungumza naye na kusema kuwa hakupendelea kushikwa hivyo.

Kisa hicho kilijiri wakati ambapo wengine katika mitandao ya kijmaii walikuwa wakimshutumu Ariana kwa kile alichokuwa akivaa kanisani wakidai kuwa nguo yake ilikua fupi mno.

Wengine walidai kwamba Ariana hakufaa kulengwa zaidi ya Askofu huyo.

Na kudai kwamba kitendo hicho cha Askofu kilihitaji kuangaziwa zaidi ya ilivyokuwa.

"Niliwakumbatia wasanii wote wake kwa waume , Askofu Ellis aliambia AP.

Kila mtu aliyekuwa amesimama nilimsalimia kwa kumshika mkono na kuwakumbatia. Hiyo ndio sababu ya kuwa kanisani, Sisi wote tuko hapa kwa upendo.

Aliongezea: kitu cha mwisho ambachpo ningetaka kufanya ni kuharibu lengo la mkusanyiko huu. Lengo letu sote ni Aretha Franklin siku ya leo.

Sio kitu pekee alichomuomba msamaha Ariana.

Awali ibada hiyo ilipoanza alifanya mzaha kuhusu jina la mwanamuziki huyo.

''Wakati nilipomuona Ariana Grande katika mpango wa ibada hii, nilidhania ni kitu kipya katika Taco Bell'', alimwambia.

Watu wengi waliona mzaha huo kuwa wa kuchekesha na kila mtu alikuwa akiuzungumzia katika ibada hiyo.

Lakini Askofu Ellis aliomba msamaha baada ya wengine kudhania kwamba ulikuwa mzaha usiofaa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad