Akipiga stori na Za Motomoto News, Aunty Lulu alisema ni ndoto yake ya muda mrefu kuzaa na Diamond hivyo ili itimie atafanya juu chini mpaka ampate hata kwa kumloga ili akikutana naye asahau hata kutumia kinga aweze kumpa ujauzito.
“Diamond amesema kwa sasa yuko makini ili asizae nje ya ndoa lakini kwangu mimi nitamloga mpaka aweze kuzaa nami kwa kuwa ni muda mrefu nina ndoto hiyo na hakuna kitakachonizuia maana namwamini sana mganga wangu,” alisema Aunty Lulu.