Aunty Lulu Amdondoshea Mate Diamond

Aunty Lulu Amdondoshea Mate Diamond
Msanii wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama Aunty Lulu amefunguka na kudai anataka sana kuzaa na msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Aunty Lulu amesema kuwa ingawa anajua itakuwa ngumu kwa yeye kuzaa na Diamond kwa sasa kutokana na Msanii huyo kusema amejifunza kutumia kinga ili kuepuka watoto wa nje lakini yuko tayari kutafuta mganga wa kumloga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aunty Lulu amesema ni ndoto yake ya muda mrefu kuzaa na Diamond hivyo ili itimie atafanya juu chini mpaka ampate hata kwa kumloga ili akikutana naye asahau hata kutumia kinga aweze kumpa ujauzito.

Diamond amesema kwa sasa yuko makini ili asizae nje ya ndoa lakini kwangu mimi nitamloga mpaka aweze kuzaa nami kwa kuwa ni muda mrefu nina ndoto hiyo na hakuna kitakachonizuia maana namwamini sana mganga wangu“.

Kwenye Interview aliyofanya mwezi uliopita Diamond alidai kuzaa na Hamisa ilikuwa ni kosa hivyo amejifunza kutumia kinga anapokuwa na michepuko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad