Baba Amuua Mwanae Kwa Sumu na Kisha Kumfukia Porini


Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Isitu Wilayani Mbarali, Geofrey Emilio Mwanganga(21) kwa kumuua mtoto wake, Prince Geofrey Emilio(5)

Mtuhumiwa anadaiwa kumuua mwanae kwa kumnywesha sumu (haijafahamika aina yake) na kisha kwenda kumfukia porini

Agosti 28, baba huyo alikwenda nyumbani kwa mkewe alikokuwa anaishi baada ya kutengana na kumchukua mtoto huyo kwa nguvu bila kibali cha mzazi mwenzake

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa, alidai mtoto alikuwa amempeleka kwa ndugu zake huko Makete Mkoani Njombe lakini baadae alikiri kuwa amemuua mtoto na kumtupa porini

Aidha, chanzo cha tukio hili ni mtuhumiwa kuhisi mtoto (marehemu) si wake bali amebambikiwa mtoto wa mwanaume mwingine
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad