Baraka The Prince: Sjawahi Kufikiria Kutoka Kimapenzi na Wema Sepetu

Baraka The Prince: Sjawahi Kufikiria Kutoka Kimapenzi na Wema Sepetu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo mwenye 'hit song' ya 'sina', Baraka The Prince amedai hajawahi kufikiria kutoka kimapenzi na mrembo Wema Sepetu licha ya kuwa ni miongoni mwa wanawake wanaomvutia kutokana na muonekano wake aliokuwa nao.

Baraka amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye FRIDAY NIGHT LIVE inayorushwa EATV kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 3:00 usiku hadi 5:00 usiku, baada ya kupita takribani siku tatu tokea alipohusishwa katika 'vichambo' vya mwanadada mkosoaji wa mtandaoni, Mange Kimambi kuwa alishawahi kutoka kimapenzi na Wema Sepetu ila wenyewe wanafanya siri juu ya hilo.

"Kutokana na heshima tuliyowekeana na Wema, sijawahi kufikiria kutokana naye kimapenzi, na hata kama ikitokea yeye mwenyewe akaniambia amenipenda basi itategemeana na mimi nitakuwa katika 'mood' gani. Mapenzi hayajawahi kuwa na 'level' na kila mtu huwa na 'choice' yake katika kumtaka mwanamke. Kiukweli Wema ni mzuri na ananivutia kutokana na muonekano wake lakini haina maana kuwa nimetoka naye kimapenzi", amesema Baraka.

Aidha, Baraka amedai kwa upande wake kuwa hana vigezo vingi katika kujihusisha na mwanamke katika mahusiano, ila kikubwa huwa anaangalia tabia ya mtu kwa kile alichodai kwamba mambo mengine wanaweza kurekebishana kutokana na vile anavyohitaji.

"Mimi huwa sina 'type' kwamba mwanamke awe hivi au vile maana type sio tabia ya mtu. Kwa hiyo huenda mimi na Wema hatujakaa sana kwamba tuna 'enjoy' na kujuana tabia kiundani zaidi ili kupelekea kunivutia kutoka naye kimapenzi", amesisitiza Baraka.

Kwa upande mwingine, Baraka The Prince amedai hana ushkaji wowote na Mange Kimambi na wala hajawahi ku-chat naye, ila anashangazwa kwa yeye kumuhisha katika masuala ambayo hayajui na wala hajawahi kuyafanya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad