Barnaba amgomea Steve Nyerere kuhusu kwenda kuloga


Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amedai haitokuja kutokea katika maisha yake kujihusisha na vitendo vya imani za kishirikina, ili kazi zake za sanaa ziweze kuonekana na watu wengi pamoja na kufika mbali zaidi. 

Barnaba ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV, baada ya kupita takribani siku tano tokea muigizaji Steve Nyerere alipomshauri ajaribu kutumia masuala ya ushirikiana yaani kuroga , kwa kile alichokidai kuwa anaimba vizuri lakini hana nyota kama walivyo wasanii wengine. 

"Steve ni kaka yangu pia nina muheshimu kwa kila anachokifanya ila kamwe siwezi kuvunja nazi katika maisha yangu, kwasababu nimelelewa na kukulia kwenye maadili bora ya dini hivyo nina muamini Mungu kuliko kitu chochote", amesema Barnaba . 

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema kuwa "kwa yoyote atakaye nishauri juu ya jambo hilo ashindwe kwa jina la Yesu, siwezi kuloga na haitoweza kuja kutokea. 'Speed' na uwezo wangu ni mkubwa sana huenda watu wengi sio mashuhuda wa haraka pia ninaamini kuwa muda ukifika kila kitu kitaonekana. Hatuwezi watu wote tukawa katika nafasi aliyoitaja au kuiwaza yeye". 

Mbali na hilo, Barnaba amesema hana mashaka na Steve Nyerere juu ya mafaniko yake, kwa madai ana muomba sana Mungu katika kufanikisha mambo yake nasio katika uchawi licha ya kuwa amepigwa vita sana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad