Barua ya Saed Kubenea Kujiuzulu Chadema Yaibua Mjadala

Barua  ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kuomba kujiuzulu imezua mjadala mzito ndani ya chama hicho.

Kubenea anadaiwa kuandika barua kuomba kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, jambo ambalo linaonekana kuleta mgongano na kurushiana mpira.

Wakati mjadala huo ukishika kasi hadi sasa mbunge huyo hajakubali wala kukataa kuhusu barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji ambaye anasema pindi itakapomfikia ataifanyia kazi haraka.

Barua hiyo ya Agosti 28 mwaka huu ilianza kusambaa mitandaoni juzi, ambapo Kubenea alikuwa akitoa utetezi wake kutokana na kuandikiwa barua na na Katibu Mkuu wa chama hicho akitakiwa kujieleza kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kusababisha migogoro kupitia mitandao ya kijamii.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu MB/U/CDM/018/1  kwenda Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Kubenea alitakiwa kujibu tuhuma tano dhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk. Mashinji alikiri kuona barua ya mbunge huyo kupitia mitandao ya kijamii, huku akiweka wazi kwamba pindi itakapomfikia ataifanyia kazi kwa haraka.

“Barua hiyo kama ambavyo umesema mwandishi ipo mitandaoni mimi bado sijaiona na kama nikiiona nitaifanyia kazi,’’alisema Dk. Mashinji.

Katika kile kinachooneka kuwa ni kukosekana kwa ufafanuzi wa kina Kubenea alikiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ikimtaka kujieleza  kutokana na kikao cha Kamati Kuu (CC) iliyokutana Julai 7 na 8 mwaka huu.

Katika sehemu ya majibu ya Kubenea kwa Katibu Mkuu alieleza kukiri kupokea barua iliyoelekezwa kwake  Julai 19  mwaka huu 2018 yenye Kumb. Na. C/HQ/K/PWN/MG/30/8, kuhusu “KUJIELEZA KWA KATIBU MKUU”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad