Bobi Wine Aonyesha Jeuri ya Pesa.... Awamwagia Mamilioni Vijana wa Jimbo Lake

Bobi Wine Aonyesha Jeuri ya Pesa.... Awamwagia Mamilioni Vijana wa Jimbo Lake
Mwanamuziki na mbunge nchini Uganda, Bobi Wine amemkejeli rais Yoweri Museveni, kwa kutoa mchango wa dola 26,000 ambazo ni sawa na milioni 59 za kitanzania kwa vijana katika eneo bunge lake mjini Kampala.



Kwa mujibu wa ripoti katika televisheni ya NTV Uganda, Bobi Wine amesema ”Kwa kuwa serikali haina la kuwaambia watu, sasa imegeukia kuwanunua-wakiona hamtishwi na risasi wanawarushia pesa”



Bobi pia amesema kuwa ”Utawala hauamini kuwa mtu anaweza kuzungumza na watu bila kuwarushia pesa” Mwanasiasa huyo anadai kuwa serikali ilijaribu kuipatia pesa familia ya dereva wake aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agost 13.Gazeti la Daily Monitor pia limeangazia madai hayo likisema familia ya dereva huyo aliyeuawa ilikataa kupokea pesa hizo.



Bobi Wine pia alidai kuwa ni yeye aliyekuwa analengwa katika kisa cha kupigwa risasi na kuuawa kwa dereva wake Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad