Bobi Wine: Kurejea Uganda Jumatatu Baada ya Kupata Matibabu Marekani

Bobi Wine: Kurejea Uganda Jumatatu Baada ya Kupata Matibabu Marekani
Mbunge wa Kyandodo Mashariki mwa Uganda, Robert Kyagulanyi ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini humo ajulikanaye kama Bobi Wine anatarajia kurudi nchini Uganda hapo Jumatatu akitokea nchini Marekani ambapo alienda kupata matibabu baada ya kupigwa na vyombo vya dola.

"Nitarejea nyumbani siku ya jumatatu,licha ya kuwa bado nna hofu lakini Uganda ndio nyumbani ambapo familia yangu na watu wangu wapo.Nina wasiwasi lakini waganda milioni 44 nao wana hofu hivyo lazima nirudi," Wine alibainisha hayo wakati akihojiwa na gazeti la Mail na Guardian

"Unaweza kukutana na kitu chochote Uganda,na hata ukiangalia historia ya wapiganaji wengi wa ukombozi wamekuwa wakikamatwa wakati wa ujio wao na mimi sina tofauti na wao hivyo nnatarajia chochote kunikuta wakati nitakaporejea"Bobi Wine alisisitiza.

Wine ambaye aliondoka nchini Uganda mwanzoni mwa mwezi septemba kwa ajili ya matibabu ameeleza pia kuwa ali yake kwa sasa inatengemaa .

Bobi Wine alikamatwa tarehe 13 Agosti baada ya mkutano wa kampeni kaskazini-magharibi kwenye mji wa Arua ambapo kuna madai kuwa msafara wa rais ulitupiwa mawe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad