Bobi Wine Kutua Leo Uganda Polisi Wapiga Stop Watu Kwenda Kumpokea

Bobi Wine Kutua Leo Uganda Polisi Wapiga Stop Watu Kwenda Kumpokea
Hatimaye msanii wa muziki nchini Uganda, Bobi Wine leo Septemba 20, 2018 anatarajiwa kuwasili nchini humo akitokea Marekani alikokuwa anatibiwa kwa wiki tatu zilizopita.

Bobi Wine amesema anarejea Uganda akiwa na amani na uhuru wa kufanya kile anachokiamini, huku akishangazwa na taarifa ya jeshi la polisi nchini humo kuwakataza wananchi waliopanga kumpokea.

Jana Jeshi la Polisi nchini Uganda, kupitia kwa msemaji wake, Emilian Kayima lilitangaza kuwa hakuna watu watakaoruhusiwa kumpokea Bobi Wine isipokuwa familia yake tu.
Bobi Wine alienda kutibiwa Marekani baada ya kupigwa na Jeshi la nchi hiyo kwa tuhuma za kuchochea vurugu kwenye uchaguzi mdogo mjini Arua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad