Bocco, Mkude, Kapombe, Feitoto Warejeshwa Kikosini

Bocco, Mkude, Kapombe, Feitoto Warejeshwa Kikosini
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha timu hiyo kitakachopambana na Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya AFCON nchini Cameroon.


Katika kikosi hicho kilichotangazwa hii leo, wamerejeshwa baadhi ya wachezaji wa Simba waliosimamishwa na baadaye kusamehewa kufuatia kuchelewa kuripoti kambini kujiandaa kwaajili ya mchezo dhidi ya Uganda ambao uliisha kwa sare ya bila kufungana nchini Uganda.

Wachezaji hao waliorejeshwa kikosini ni, John Bocco, Jonas Mkude, Shomari Kapombe pamoja na kiungo wa Yanga, Feisal Salum huku Shiza Kichuya na Hassan Dilunga wakiachwa katika listi hiyo.

Listi ya kikosi cha wachezaji 30 kilichotangazwa na kocha Emmanuel Amunike ni pamoja na, Aishi Manula, Jonas Mkude, Shomari Kapombe na John Bocco wa Simba, Frank Domayo, David Mwantika, Agrey Morris, Mudathir Yahya, Yahya Zayd na Abdallah Kheri wote wa Azam Fc, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Beno Kakolanya, Andrew Vicent na Feisal Salum wa Yanga.

Wengine ni Kelvin Sabato na Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar, Paul Ngalema na Ally Mtoni wa Lipuli Fc, Mohamed Abdurahman wa JKT Tanzania pamoja na Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons.

Wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa katika kikosi ni nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta(Genk ya Ubelgiji), Simon Msuva(Difaa El Jadida ya Morocco), Himid Mao(Petrojet ya Misri), Abdi Banda(Baroka Fc ya Afrika Kusini), Shaban Chilunda na Farid Musa(Tenerife ya Hispania), Rashid Mandawa(DBF ya Botswana) pamoja na  Hassan Kessy(Nkana Rangers Fc ya Zambia).

Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Oktoba Mosi ambayo itakuwa ni siku moja baada ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaopigwa 30, Septemba tayari kujiandaa na mchezo wa ugenini dhidi ya Cape Verde utakaochezwa 12, Oktoba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad