Tangu aliposhinda pambano lisilo la ubingwa dhidi ya Sam Eggington nchini Uingereza, mwanamasumbwi raia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo ameweza kujitangaza ndani na nje ya mipaka, na hatimaye amepata dili nyingine la pambano nchini Ujerumani.
Hassan Mwakinyo, aliyepigana mapambano 14 mpaka sasa akishinda 12 na kupoteza mapambano mawili pekee, huku michezo nane kati ya 12 aliyoshinda ameshinda kwa KO, ambapo hivi sasa amepanda hadi nafasi ya 16 kutoka 174 ya viwango vya uzito wa kati duniani.
Bondia huyo amepata nafasi ya kupigana pambano la ubingwa ambapo anatarajia kupambana bondia, Wanik Awdijan kuwania ubingwa wa IBF kwa uzito wa kati, pambano iltakalofanyika 20 Oktoba 2018 nchini Ujerumani.
Wanik Awdijan (23) ni raia wa Ujerumani ambaye ana rekodi ya kucheza mapambano 24 mpaka sasa na kushinda mapambano 23 akipoteza pambano moja pekee dhidi ya Kevin Thomas Cojean kwa TKO mwaka 2014.
Mapambano tisa kati ya 23 ambayo Awdijan ameshinda, ameshinda kwa TKO na anakamata namba tatu kati ya mabondia 68 wa uzito wake nchini Ujerumani. Bondia huyo ana sifa ya kutumia zaidi mkono wa kushoto katika mapambano yake.
Pambano hilo litamfanya kukwea katika nafasi kubwa ya ubora wa ngumi duniani endapo atashinda pambano hilo kutokana na mpinzani wake huyo kumzidi rekodi za pambano aliyocheza na kushinda mpaka sasa