Bondia Hassan Mwakinyo Apata Mfadhili wa Nguvu


Baada ya kumtwanga bondia kutoka England, Samm Eggington, Mwekezaji wa klabu ya Simba amempa ufadhili Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo kuelekea pambano lake dhidi ya Wanik Awdijan.

Mo ameamua kuwekeza nguvu zake kifedha kwa Mwakinyo ili kumtengenezea mazngira ya kuzidi kufanya vizuri ambapo atakuwa anachuana na Awdijan kutoka Ujerumani Oktoba 20 2018.

Taarifa hizo zimekuja mara baada ya Mwakinyo kukosa watu wa kumuwezesha kupata maandalizi ya kutosha na sasa bila shaka ndoto yake imezidi kunawili kutokana na kupata nguvu kwa Bilionea huyo kijana ndani ya Afrika.

Mwakinyo atakuwa na kibarua hicho ambacho kitafanyika huko Ujerumani tayari kuweka rekodi nyingine itayoweza kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad