BREAKING: Hatimaye Zoezi Lakamilika, MV Nyerere Yatua Nchi Kavu


Hatimaye zoezi la kukikwamua kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara na kuua mamia a watu limekamilika baada ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi kwa kutumia tingatinga kukivuta kivuko hicho hadi kwenye mwalo wa Bwisya ambapo kitakabidhiwa kwa TEMESA kwa ajili ya matengenezo.

Zoezi hilo limekamilika leo asubuhi, Ijumaa Septemba 28, 2018 na sasa kazi iliyobaki ni kuondoa maji na kuweka taratibu za kukikarabati ili kirudi kwenye hali yake ya awali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad