Akiongea na wanahabari leo, Hashim Issa amesema wao kama CHADEMA hawafurahishwi na kinachoendelea ndani ya CUF na endapo kitakufa wao watajiimarisha zaidi Zanzibar na kumpa nafasi Maalim kugombea Urais visiwani humo kupitia CHADEMA.
''CHADEMA na CUF ni kitu kimoja, kwa hiyo CUF ikitetereka sisi tutaimarika zaidi na kushika nguvu Zanzibar na sisi tutawakaribisha wagombea wote Zanzibar wachukue fomu na kugombea kupitia CHADEMA na hiyo ndio mipango yetu kama Baraza la Wazee'', amesema.
Aidha amesisitiza kuwa sababu kuu ya msingi ya CHADEMA na CUF kuungana ilikuwa ni kukubalika kwa CUF kwa zaidi ya asilimia 80 katika visiwa vya Zanzibar lakini kwasasa CCM wakifanikiwa kuipangua CUF Zanzibar CHADEMA haitashindwa kuchukua hatamu huko.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo amesema wao kama Baraza la Wazee wataendelea kuhakikisha CHADEMA inaendelea kuimarika nchini kote hususani Zanzibar kwasababu wameona CUF inaweza kuvunjika kutokana na hali ilivyo sasa.