Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema huo ni Uamuzi wa Kamati ndogo ya Kamati Kuu iliyokaa jana Septema 18 jijini Dar kutafakari mwenendo mzima wa uchaguzi
Amesema sababu mojawapo ni kukiukwa kwa Katiba katika chaguzi zilizopita za marudio ambapo kuna baadhi ya watu walinyimwa haki yao ya msingi ya kupiga kura
Sheria inasema katika zoezi moja la uchaguzi mkuu mpaka uchaguzi mwingine mkuu, wapiga kura wataandikishwa mara mbili lakini mara ya mwisho wapiga kura wameandikishwa nchini ilikuwa Agosti 2015
Hivyo basi, wale wote ambao wamefikisha miaka 18 kuanzia Novemba 2015 hawajapewa haki yao ya msingi ya kupiga kura katika maeneo yaliyokuwa na uchaguzi wa marudio
Aidha, amesema "Tume haitekelezi majukumu yake kwa mujibu wa Katiba kwa sababu Serikali ya CCM inahofia sana kuwa wapiga kura wengi ni vijana wanaounga mkono vyama vya mageuzi"