Chadema Yapambana Kutafuta Dhamana ya Makene

Chadema Yapambana Kutafuta Dhamana ya Makene
Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) wanaoishi nje (Diaspora) wamesababisha kushikiliwa na jeshi la polisi Mkuu wa Kitengo cha Habari wa chama hicho Tumaini Makene kwa kuendesha blog ya Chadema bila kusajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Pia hatma ya dhamana ya afisa habari huyo wa CHADEMA inatarajiwa kujulikana leo kama ataruhusiwa kwa dhamana au kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na www.eatv.tv mapema leo asubuhi wakili wake Fred Khiwelo amesema “Makene anatuhumiwa kwa kuendesha blogu ya chadema ambayo imesajiliwa na wanachama wa Chadema wanaoishi nje ya nchi licha kwenye blogu hiyo kuonekana jina lake.”

“Bado Tunafatilia dhamana ya mtuhumiwa kwa hiyo tunategemea leo na tumezungumza nao polisi wakishindwa kumpa dhamana wamfikishe mahakamani.”ameongeza wakili Khiwelo.

Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia Makene kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana blog iitwayo Chadema.blogspot.com pamoja na maudhui yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad