Chadema yataka Takukuru ichunguze wabunge wake Kuhamia CCM

Chadema yataka Takukuru ichunguze wabunge wake Kuhamia CCM
Uamuzi wa aliyekuwa Mbunge Serengeti, Ryoba Chacha kutangaza kujiuzulu ubunge na kuhamia CCM, umekifanya chama chake cha zamani cha Chadema kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kuona kama kuna aina mpya ya rushwa ya madaraka ambayo inawavuta wabunge wengi wa chama hicho kukimbilia chama tawala.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

“Wabunge wamekuwa wakiahidiwa kupewa ubunge wao baada ya kuhamia CCM, hiyo ni aina nyingine ya rushwa, Takukuru waingilie kati suala hilo na kuchukua hatua,” amesema.

Mrema alidai suala la wabunge na madiwani wa Chadema kutimukia CCM haliwapi shida kwa sababu wanajua mazingira yalivyo sasa.

Alidai Mbunge huyo (Ryoba) amefanya kile alichokisema wakati wa mkutano wa Rais Magufuli huko Serengeti na kwamba hawashangazwi na uamuzi wake kwa sababu yeye siyo wa kwanza kuhama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad