Chemical 'Hakuna Wasanii Wenye Vipaji kwa Sasa, Wanatengenezwa'

Msanii wa kike, Chemical amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu vipaji vya sanaavilivyopo bong na kusema kuwa vipaji  vya kutoka moyoni vilikuwepo zamani lakini sio sasa hivi kwa sababu kwa sasa wengi wamekuwa wakitengenezwa.

Chemical anasema kuwa kuna watu wamekuwa wakijifanya wanajua kuimba lakini hakuna kitu na hii inamfanya awaonee  huruma sana wasanii chipukizi ambao wana vipaji lakini hawawezi kusaidiwa mpaka watoe pesa ili kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Kuna watu wanaharibu sana sanaa sasa hivi, unakuta mtu hajui kuimba nakaa studio wiki nzima anarecodi nene moja lakini mwisho wa siku ana mlipa producer na producer hasemi chochote tofauti na zamani msanii akiingia studio anaimba wimbo wote  bila kuogopa chochote lakini sasa hivi imekuwa changamoto sana. -Alisema Chmeical alipokuwa akiongea na EATV

Chemical anawaomba wadau wa muziki kuangali hillo hasa kwa sababu wasanii wengi wanaozalishwa sasa hivi ni wabovu sana na ndio wanaoharibu sanaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad