Parma 1 Juventus 2, unawaza nini unaposoma ubao wa matokeo unasoma namna hiyo? Moja kwa moja utakimbilia kuuliza Ronaldo amefunga, na jibu la hajafunga linakujia.
Ni kweli bwana Mario Madzukic kama kawaida amesimamia show hii leo pamoja na Blaise Matuidi wamefunga mabao ya Juventus vs Parma na Gervinho akafunga la Parma na kumfanya Cr7 kutofunga katika mechi 3 za mwanzo Serie A.
Suala la kuhuzinisha kuhusu Ronaldo ni hizi timu tatu walizokwishacheza nazo, hizi ni timu ambazo kweye makaratasi zonaonekana ni nyepesi sana.
Hivi kwa mfano Chievo, msimu uliopita walimaliza nafasi saba kutoka mwisho tena walimaliza msimu wakiwa na goal difference ya mabao 23, Ronaldo hakuwafunga.
Lazio, kama hujui tu nikuambie Lazio msimu uliopita katikaashindano yote walifungwa mabao 70, ni timu ambayo ina ulinzi dhaifu lakink Ronaldo hakufunga.
Parma hawa hadi mwaka 2016 walikuwa Serie D huko, 2015 walikumbwa na tatizo kubwa la kipesa wakafilisika, na mwaka huu ndio wamepanda Serie A, Ronaldo kawapigia mashiti 23 hajafunga.
Kwa kumalizia tu nkuambie tangu Cristiano Ronaldo aondoke Real Madrid, Karim Benzema amefunga mara 4, Gareth Bale mara 3, Cristiano Ronaldo 0, anakwama wapi?