UNAAMBIWA Dar es Salaam ndilo Jiji la pili kwa utajiri Afrika Mashariki baada ya Nairobi, huku nchi ya Tanzania ikiwa taifa la nane kwa jumla ya utajiri wa raia wake kwa Bara zima la Afrika na Kenya inashikilia nafasi ya tano.
Kwa mujibu wa ripoti ya New World Wealth pamoja na benki ya AfrAsia nchini Mauritius, utajiri wa Dar es Salaam wenye thamani ya $25 bn mwaka 2017 umetokana kukuwa kwa viwango vya utajiri wa watu binafsi (HNWIs) na mapato yanayoingia katika sekta ya starehe Barani Afrika kama hoteli na vivutio vingine.
Hii ni hatua iliyopigwa ikilinganishwa na utajiri wa thamani ya Dola bilioni 23 kwa nchi nzima ya Tanzania mnamo mwaka 2011.
Kwa jumla, ripoti hiyo inakadiria kuwa sekta hiyo ya starehe barani Afrika imechangia takribani dola bilioni 6.0 za mapato mnamo 2017.
Ongezeko la utajiri, mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, isipokuwa Burundi, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeimarika pakubwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mauritius inaongoza kwa ukuaji wa asilimia 192 ikifuatwa na Ethiopia iliyokuwa kwa asilimia 190. Jumla ya majiji makubwa Afrika ni 12 huku Nairobi ikiwa nafasi ya sita na Mombasa ni mji wa 23 kwa utajiri Afrika.
Baada ya hapo, mataifa ya Afrika Mashariki yanafuata yakiongozwa na Rwanda (74%), Kenya (73%), Tanzania (66%), na Uganda (53%). Na takwimu hii inajumuisha vitu kama; Magari na nguo za kifahari, ndege za kibinfasi, boti na hoteli zinazomilikiwa.
Afrika Kusini ndiyo kivutio kikuu cha utalii Afrika, lakini Tanzania inasifika pakubwa kwa vivutio vikiwemo; Mbuga za Ngorongoro na Serengeti. Na hii ni kama ilivyo kwa mfano wa Masai Mara nchini Kenya, na safari za kuzuru milima ya Virunga na msitu wa Bwindi nchini Uganda kwenda kutazama sokwe.
Kuihusu Tanzania
Kwa mujibu wa Jacque Morisset, Mwanauchumi Mkuu wa Benki ya Dunia, wakaazi wa Dar es Salaam kwa jumla wanaonekana kumiliki mali zaidi ya watu wanaoishi nje ya mji huo na hasaa katika maeneo ya mashambani.
Dar es Salaam ni mojawapo ya miji inayotazamwa kukua kwa kasi duniani.
Mji Utajiri kwa Mabilioni ya Dola
1. Johannesburg 276
2. Cape Town 155
3. Cairo 140
4. Lagos 108
5. Durban 55
6. Nairobi 54
7. Luanda 49
8. Pretoria 48
9. Casablanca 42
10. Accra 38
11. Abidjan 27
12. Dar Es Salaam 25
13. Alexandria 25
14. Kampala 16
15. Windhoek 13
16. Abuja 13
17. Addis Ababa 13
18. Marrakesh 11
19. Tangier 11
20. Lusaka 10
21. Maputo 10
22. Gaborone 9
23. Mombasa 8
Mji wa Dar es Salaam una mali zinazomilikiwa na watu binafsi yenye thamani ya mamilioni ya dola ukifuatwa na Kampala na Mombasa, uliopo Pwani ya Kenya ambayo ina na mali ya mamilioni ya dola, yalioekezwa zaidi katika hoteli na nyumba za mapumziko za kifahari katika fukwe za bahari.
Utajiri dhidi ya Umaskini
Licha ya haya bado changamoto inasalia katika mgawanyiko wa uchumi wa taifa unaoegemea upande mmoja zaidi. Kiwango kidogo cha matajiri ikilinganishwa na sehemu kubwa ya watu walio maskini katika mji mkuu huo.
Picha iliyopo ni ya badhi walio maskini wanaoishi katika mitaa inayokosa huduma muhimu kama maji.
Huku upande wa pili wachache walio na mali wakiwa na uwezo wa kuishi katika nyumba za ufukweni zenye thamani ya mamilioni ya dola au wengine katika mitaa ya kifahari katika wilaya zilizopo Kaskazini.
Ripoti hiyo imetathmini utajiri, starehe, mkondo wa umiliki na usimamizi wa mali Barani Afrika kati ya mwaka 2007 hadi 2017, ikitazamia makadirio ya hadi 2027. Na imefanya hesabu ya utajiri wa kila nchi kutokana na idadi ya wananchi wanaofanya kazi au kuishi ndani ya nchi hiyo.
Taifa Jumla ya utajiri wa mali kwa Mabilioni ya Dola
(Jumla ya utajiri wa taifa ni jumla ya mali ya raia wake)
Afrika Kusini 722
Misri 330
Nigeria 253
Morocco 122
Kenya 104
Angola 81
Ghana 63
Tanzania 60
Ethiopia 60
Cote d’Ivoire 46
Katika mji mkuu wa nchi jirani Kenya, Nairobi huvutia watu wenye utajiri katika masuala ya biashara na uwekezaji. Mji uliopo Pwani Mombasa una umaarufu wa kuvutia watalii katika hoteli nyingi zinazopatikana ufukweni mwa bahari hindi na maeneo yalio torathi za kitaifa na vivutio vikuu duniani.
Nchini Uganda na Rwanda, utajiri wa watu binafsi umetajwa kuogezeka kwa 6% huku Tanzania ikiwa ni 5% kwa jumla nchini.
Dar Es Salaam Ndilo Jiji la Pili kwa Utajiri Afrika Mashariki
0
September 18, 2018
Tags