Wadau,
Napenda kutoa wazo au ushauri au msukumo au kuishawishi serikali kwamba daraja hili la mto Wami sasa linatutia aibu na lijengwe kisasa sasa maana kwa miaka hii 50 ya Uhuru hatupashwi kuona magari yakisubiriana kupishana juu ya daraja
Mheshimiwa Rais wangu na Serikali yako embu fanyeni jambo juu ya hili daraja sasa maana ni kiungo muhimu kwa mikoa hii ya Kaskazini na nchi jirani na ni kiungo muhimu kwa uchumi wetu.Hili daraja likitengenezwa kisasa litasaidia mapato kwa nchi yetu. Litatoa hofu kwa watumiaji maana palivyo panatisha na ikizingatiwa kule chini kuna mamba haswa.
Najiuliza kama serikali imeweza kujenga daraja la Kigamboni tena juu ya bahari je hili la Wami ni nini mpaka ishindwe nikijaribu kufanya tathmini ya macho naona kama ku-cross pale hakuna hata mita 500 so hata gharama yake ya ujenzi yaweza kuwa ndogo zaidi kuliko ile ya daraja la Kigamboni au daraja la Mkapa kule Kusini.
Kuna manufaa makubwa yanayoweza kupatikana kwa ujenzi huu both Economically, Socially na hata politically.
Shime Serikali ya awamu ya tano embu fanyeni mabadiliko katika daraja hili lililopo kilomita kadhaa kutokea Chalinze kuelekea Arusha na mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata (kwa wasiolijua).
Serikali ya CCM chini ya Jemedari wangu Rais Magufuli najua mtanisikiliza wazo langu na mtalitendea kazi.
Mafie Jr/JF