Davido Aijia juu Tume ya Uchaguzi Nigeria, Ataka Wananchi Wakatae Matokeo ya Uchaguzi ‘Miaka Mitatu Hakuna Maendeleo’


Msanii wa muziki nchini Nigeria, Davido amewaomba wafuasi wa chama cha kisiasa nchini humo cha  Peoples Democratic Party (PDP) wapingane na kauli ya Tume ya Uchaguzi nchini humo.


Davido akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mapema wiki iliyopita
Davido amesema matokeo ya uchaguzi wa Gavana katika jimbo la Osun nchini humo, yanaonesha mjomba wake Ademola Adeleke kupitia chama cha PDP, ameshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi huo lakini Tume ya Taifa inataka kubadilisha matokeo hayo na kutaka uchaguzi urudiwe tena.

“They are planning now to declare the election inconclusive as a result of cancellation and violence in some p u bc the margin is too close, PDP must fight this injustice. We must come out to say no to this daylight robbery !!!! @inecnigeria”ametweet Davido.

Davido aliendelea kumpigia upatu Mjomba wake kwa kusema kuwa Chama Tawala nchini Nigeria cha APC kisichukulie poa kupanga matokeo kwani wananchi wa jimbo la Osun wamechoshwa na chama hicho na hawapo tayari kuishi maisha ya tabu kwa miaka mitatu.



Licha ya Tume ya Taifa nchini humo (INEC) mpaka sasa kutotangaza matokeo ya uchaguzi, matokeo yanaonesha kuwa Mjomba wake na Davido anaongoza kwa kura 254,698 dhidi ya mpinzani wake wa Chama tawala cha APC kura 254, 345 kwenye uchaguzi huo.

Mzee Ademola Adeleke ni mjomba wake kabisa na Davido na watoto wake ni B-Red na Sina Rambo ambao wote wanafanya kazi na Lebo ya muziki ya DMW ya Davido
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad