Diamond awajibu wanaobeza Style Yake ya Rasta ‘Nimeamua Kubadilisha Muonekano’

Diamond awajibu wanaobeza style yake ya rasta ‘nimeamua kubadilisha muonekano’
Rais wa WCB Diamond Platnumz Jumatatu hii amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushare picha inayomuonyesha akiwa na muonekano mpya wa mwele ambazo zimesukwa mtindo wa rasta.



Wadau wengi katika mitandao ya kijamii wanadai mtindo huo niwa kike kutokana na msuko huo kuacha nywele sehemu ya nyumba.

Bongo5 ilizungumza na Diamond kuhusiana na tukio hilo ambapo amesema yeye ameona yupo sahihi ndio maana ameamua kufanya hivyo.

“Nimeamua tu kubadilisha kidogo muonekano, baadae nitabadilisha tena” alisema Diamond.

Wiki chache zilizopita mumbaji huyo alishambuliwa mitandaoni baada ya kuvaa kikuku na baada ya kuhojiwa alisema asipangiwe kitu cha kufanya katika maisha yake.

Diamond afunguka kuhusu muonekano wake wa nywele “Nimeamua tu kubadilisha kidogo muonekano, baadae nitabadilisha tena”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad