Diamond Platnumz Amshukia Hamisa Mobetto "Unaonekana wewe Haushindwi Kumuua Mama yangu Kama Unawaza Nikupe Nyumba"


Msanii wa muziki Diamond Platnumz amefunguka kuzungumzia sakata la kutaka kurogwa na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto ikiwa ni siku chache toka audio inayodaiwa kuwa ya mrembo huyo isambae mtandaoni akisikika kuzungumza na mtu anayeadaiwa kuwa ni mganga kuhusu familia ya rais huyo wa WCB.

“Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe,” alisema Diamond kupitia Refresh ya Wasafi TV.

Aliongeza,
”Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi,”

 Wiki hii dada wa Diamond Platnumz, Esma aliandika ujumbe mrefu kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kwamba wameandaa voice note kwaajili ya kumchafua Hamisa Mobetto

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kabla ya kuanza kuamini ushahidi wa kutosha ni lazima. Bila ushahidi wa kutosha wengi wsliamini na kumiminika kwa kasi ya AJABU kuelekea Loliondo kwa babu kutafuta uponyaji, u should wa kisayansi ulikuja baadaye sana kuwa kikombe hakukuwa dawa ya ukimwi.

    Bila ushahidi wa kutosha wengine wsliamini dkt shika alijisalimisha kutoka kwa wstekaji nyara wake huko Urusi kwa kufungua mlango taratibu ili asimwamshe mtekaji aligelala baada ya kukidunga ulevi na kwa kushikilia kengele. Walisahau ukweli kuwa vidole vya dkt shika mikono yote miwili vilikuwa vimekatwa kikatili, hivyo ni wazi maumivu yalikuwa makali na nahisi ilikuwa imevimba na kupotelewa na uwezo wa kukunja na kushika chochote ikiwemo kushikilia kengele au kitasa cha mlango. Kwa hali hiyo, kama alijinasua basi waliomnasua walimfuTa na ile damu ndani ya chumba pengine ni yaympambano mkali kati ya waliomshikilia na waliomsadia.

    Mazungumzo ya siri kwa njia ya simu yaliyorekodiwa? Na nani? Mganga alieksposi mazungumzo na mteja ili kuharibu business yake? Au ili amuuzie Mr Diamond mazungumzo hayo kwa bei kubwa zaidi kwa kuwa Diamond ni tajiri anayefahamika nchini?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad