Dkt Anthony Mwandulami: Mtanzania Anayejijengea Kaburi Lake la Kifahari Njombe

Dkt Anthony Mwandulami: Mtanzania anayejij engea kaburi lake la kifahari Njombe
Umewahi kujiuliza utazikwa wapi baada ya kufa? Mwanamume mmoja nchini Tanzania ameamua hataki utata kuhusu hatima yake baada ya kufa.

Dkt Anthony Mwandulami mkaazi wa Njombe nyanda za juu Kusini mwa Tanzania ameshaanza kujijengea kaburi lake tayari. Mwandulami ambaye pia ni mganga wa tiba asilia, anasema kaburi hilo ambalo amekuwa akilijenga kwa takriban miaka minane sasa.

Alimwambia mwandishi wa BBC David Nkya kwamba sababu kuu inayomfanya kujijengea kaburi hilo ni kuihifadhi historia yake baada ya kifo.

Kaburi hili si tu limeleta mshangao kwa wakazi wa eneo la Njombe, lakini pia linawashtua wengi nchini kote.



Anthony Mwandulami: Mwanamume anayejiandalia kaburi lake Tanzania
Lina urefu wa mita kumi na mbili kwenda chini na limejengwa kwa mfumo wa jengo la ghorofa.

Lakini Waafrika wengi hawana tabia ya kufikiria watazikwa wapi ukiachilia mbali kujijengea makaburi wangali wako hai, kulikoni kwa Mwandulami?

Kaburi
"Kaburi hili nimeamua kulijenga, nimeona si vizuri sana kutokana na shughuli zangu nilizozifanya hapa Tanzania na nilivyowasaidia Watanzania, halafu nikapotea tu. Na wakati huo huo nimeona nina uwezo wa kujitengenezea sehemu ya kuhifadhi mwili wangu. Nikaona bora nitengeneze. Kaburi hili nimeliandaa kwa ajili ya kupumzisha mimi na wake zangu," anasema.

"Ni muhimu sana kwa sababu siwezi kusahaulika na wajukuu zangu pamoja na watakaozaliwa na familia yangu watakuja kujua kwamba huyu ni nani na alifanya nini kwenye familia yetu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad