Dogo Janja Amkumbuka Mungu

Dogo Janja amkumbuka Mungu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mume halali wa muigizaji wa filamu Irene Uwoya, Dogo Janja amefanikiwa kuwatia nguvu na ujasiri baadhi ya watu waliokwisha kata tamaa na maisha kupitia tungo za mashairi ya wimbo wake mpya ulioupatia jina la 'Imani', aliouachia usiku wa kuamkia leo.

Kupitia wimbo huo, Dogo Janja amezungumza mengi kuhusiana na hali ya maisha ya ambayo wengi wao wamekuwa wakishindwa kusonga mbele kutokana na vikwazo wanavyokumbana navyo katika harakati zao za kila siku za kutafuta riziki na hata wale waliopo kwenye mahusiano.

"Maisha ninayopitia wala sioni msaada, ni Mungu tu aliyejuu anayeniongoza hali yangu, nayaweka kifuani simwambii mtu. Nitafaulu yote kwa nia tu, barabarani jua kali, 'God i need you'. Bado naimani yote napitia.....Sina sina urafiki na ndugu yenu.... nilikuja pekee yangu bila ya wenzangu hakuna ninachohofia zaidi ya Mungu na mama yangu ndio maana nipo hapa namsujudia mengi nakwambia kuna viumbe vinaumia", Dogo Janja ameimba katika mashairi ya wimbo huo.

Kutokana na hilo, Dogo Janja amepongezwa na baadhi ya mashabiki zake kwa kuweza kubadilika kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho, huku wengine wakimshauri kuwa asipende kuyapa mapenzi kipaumbele kwa kuwa yanaweza kuhatarisha maisha yake na ufanisi wa kazi kiujumla.

"Unakipaji dogo janja lakin kwa huu wimbo umeonesha kipawa na uwezo wako wa sanaa ya muziki. Muzik mzuri... 'Congratulations' Janja", ameandika otty_ottinger

"Kadri siku zinavyokwenda unazidi kuonsha kipaji chako alichokubariki 'God even management' nzuri pia najua nyuma kuna juhudi za shemela ndio maana unazidi kuumiza mtaa Buddaboss Badman proud of you Chuganian Janjaro", ameandika Syrenees Kadri

"Wimbo mzuri sana na una mafunzo ndani yake jamani hongera sana",ameandika preciox_annie.

"Wewe kimuziki upo vizuri sana fanya muziki achana na maisha ya mapenzi kama unahisi na kuamini huyo mkewe hayupo pamoja nawe achana nae dogo wapo wengi hao", ameandika hashimuchidy.



Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii walioweza kuandamwa mitandaoni katika miaka ya hivi karibuni, kwa kusemwa vibaya juu ya mahusiano yake ya ndoa ambapo kila mmoja anazungumza lake huku wengine wakidai kijana huyo hajaoa bali ameolewa kwa kile wanachokidai amezidiwa umri mkubwa na mke wake Irene Uwoya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad