Familia ya Kijana Aliyejinyonga Moshi Yaandamana

Familia ya kijana aliyejinyonga Moshi yaandamana
Familia ya mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Rau, Emmanuel Tarimo (18) aliyejinyonga baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake a kidato cha kwanza, wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa shule hiyo kutaka kujua sababu za mwanafunzi huyo kuhojiwa hadi kupelekea kujiua.

Dada wa mwanafunzi huyo, Tedy Maro amesema anataka uongozi wa shule hiyo uwaeleze kinagaubaga kwanini walimu wa shule hiyo wamtuhumu mwanafunzi huyo wakati wao familia hawakupewa taarifa zozote kuhusu mwenendo wa tabia za mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo alijinyonga hadi kufa Septemba 4, mwaka huu nyumbani kwao Kijiji Cha Rau, mtaa wa Saba Saba baada ya kutuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi mwenzake wa kidato cha kwanza.

Mazishi ya kijana huyo yanatarajia kufanyika kesho Moshi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad