Faru Fausta Aibuka Bungeni Mbunge Ahoji Gharama ya Matunzo Yake

Faru Fausta Aibuka Bungeni Mbunge Ahoji Gharama ya Matunzo Yake
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga amesema kutokana na heshima ya Faru Fausta ambayo imeliletea faida taifa kutokana kuwa kivutio cha watalii kutoka nje ndio maana aliwekwa katika uangalizi maalum ili kunusuru maisha yake baada ya kujeruhiwa na fisi kutokana na uzee.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Septemba 11, 2018 wakati Naibu waziri huyo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Suzana Chogisasi (CHADEMA) lililohoji kuwa ni lini serikali itaanza kuwahudumia wazee wa taifa hili kama wanavyomtunza Faru Fausta kwa gharama zote anazotunzwa ili kusudi kuleta amani katika nchi?

Hasunga amesema kuwa "Wanyama wana haki sawa kama binadamu wengine, na huyu Faru Fausta kutokana na uadimu wao wa kuwepo hatarini kutoweka ndio maana tumemuweka katika ulinzi maalumu”, amesema Hasunga.

Ameongeza kuwa “Kutokana na umuhimu wake huo na jinsi alivyoingizia taifa fedha nyingi za kigeni pamoja na watu wengi kutaka kujua maisha yake ataishi miaka mingapi maana hadi sasa ana miaka 53, ndio maana tumeamua kumuweka katika ulinzi sawa na binadamu na sio kwa mba hatujali wazee na wazee wote ambao wameshafikisha miaka sitini watapatiwa matibabu bure”.

Faru Fausta alijeruhiwa na Fisi mwaka 2016 akiwa mbugani katika hifadhi ya Ngorongoro ambapo serikali ililazimika kutumia kiasi cha shilingi Milioni 1.4 kila mwezi sawa na shilingi Bilioni 64 kwa mwaka ili kumuweka katika uangalizi maalum na kwa sasa afya yake imerejea kawaida na anatumia laki 285 kila mwezi katika matumizi ya chakula.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad