Dr. Reginald Mengi Aguswa Na Mkakati Wa Rc Makonda Kusaidia Walemavu, Amuahidi Bilion 5


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu leo ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dr. Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dr. Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu.

Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora.

Kwa upande wake Naibu waziri Wizara ya Ajira, Wazee, watoto na watu wenye ulemavu Mhe. Anton Mavunde, Mbunge wa viti maalumu Mhe. Amina Molel na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyopambana kuwakwamua watu wenye ulemavu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad