Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imempa onyo la mwisho msanii wa bongo fleva na 'video vixen' nchini, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi watamchukulia sheria stahiki dhidi yake.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Juliana Shonza amesema kwamba hawata waangalia usoni wananchi pamoja na wasanii kiujumla watakao kuwa wanaenda kinyumae na sheria ya mitandao.
"Huyu Gigy Money naona bado hajaacha michezo yake kwenye mitandao, safari hii sidhani kama atapona katika huu mchakato wa kuwakamata wasanii. Lakini kupona kwake labda yeye mwenyewe abadilike na awe kama isheria ya mitandao inavyotaka. Niwasii wasanii na watanzania wote kwamba waheshimu, mila na tamaduni za kitanzania kwasababu serikali ipo macho", amesema Mh. Shonza.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema hawataacha kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii huku akisisitiza kwamba hawasita kuwachukulia hatua stahiki watu wote wanatao bainika wameenda kinyuma na matakwa ya sheria ya mitandao.