Gwajima "Kipigo Alichokipata Lowassa Monduli ni zaidi ya cha Mbwa Koko"


Gwajima amesema Kipigo cha Monduli alichopata ni kibaya mno na ni zaidi ya Kipigo Cha Mbwa Koko kiasi kwamba, kisiasa sasa anatia aibu/Huruma/Simanzi, hivyo anapaswa kusoma alama za nyakati kwani kama ni kuisoma namba hakika hii ya Monduli ni ya kufunga mwaka !!

“Hivi kweli kama umeweza kushindwa kulikomboa Jimbo moja tu tena la Nyumbani kwako, Je utaweza tena kuhimili mchaka mchaka wa nchi nzima ? Kwa hakika busara ya kawaida inakutaka upumzike na ikibidi uachane kabisa na harakati za kisiasa, baki nyumbani walau hata uwe mshauri tu kwa watu watakaohitaji ushauri wako” alisema Gwajima.

Gwajima ambaye ni Mwanasheria kitaaluma amemtaka Lowasa Kuepukana na washauri wabaya waliomzunguka kwani kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kumuingiza chaka bure mzee wa watu.

“Nadhani, Mhe. Lowasa amezungukwa na genge la wahuni na wapiga dili ndio maana wanashindwa kumpatia ushauri mzuri unaoendana na umri na heshima yake.

Mhe. Gwajima amewapongeza Wagombea wote wa CCM waliofanikiwa kupata ushindi wa kishindo

“Hongera sana wanaukonga, Hongera sana wana Monduli, Hakika nyinyi hampangiwi cha kufanya ama kweli wanaukonga na Monnduli sio wa mchezo mchezo”

Mhe. Gwajima amevipongeza vyombo vyote vya dora kwa kusimamia amani na utulivu wakati wote wa kampeni na hatimaye katika zoezi zima la uchaguzi.

Ushindi huu wa CCM katika chaguzi ndogo zilizofanyika jana ,ni ishara kubwa ya imani walionayo wananchi kwa serikali yao chini ya Mhe. Raisi wetu Mpendwa Dr. John Pombe Magufuli katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Mhe. Gwajima amempongeza Mh. Raisi Magufuli kwa kufanya mambo makubwa ya wakuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote na mda mfupi sana tangu aingie madarakani.

Mhe. Gwajima Alimpongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wake na usimamizi katika kusimamia yafuatayo:

i. Katika Ujenzi wa Bomba la mafuta HOIMA –TANGA
ii. Ongezeko Katika makusanyo ya kodi –TRA
iii. Mradi wa STIEGLERS’S GORGE MEGAWATI - 2,100
iv. Mahakama ya rushwa na uhujumu uchumi
v. Serikali kuhamia makao makuu DODOMA
vi. Elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne.
vii. Ujenzi wa Ukuta wa kulinda Madini MERERANI.
viii. Kufufua Shirika la ndege nchini.
ix. Usajili wa kuwatambua rasmi wamachinga 20,000
x. Huduma bora za tiba kwa watanzania
xi. Mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu mfano mzuri ni Flying Over ya Tazara.

Mwisho Mh. GWAJIMA amewaomba watanzania kuendelea kumunga mkono Mh. Raisin a serikali yake kwa ujumla KWANI YAJAYO YANAFURAISHA MNO.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sijamsikia mkuu akikussema vibaya. alimsema vibaya yule wa kaskazini magharibi. je unatafuta kiki kwa kumsifia. mbona wewe ni mtu wa kanisa unaingiliaje ya siasa. yaache mambo ya siasa kama walivyoshambuliwa wengine. je umeingia kwenye siasa za ccm. au wewe ni msukuma pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad