Haji Manara Afichua Siri ya Kuugua Ghafla Adai Amewekewa Sumu

Haji Manara Afichua Siri ya Kuugua Ghafla Adai Amewekewa Sumu
Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameshikwa na presha iliyopelekea kulazwa mkoani Shinyanga, hatimaye mwenyewe aweka wazi kinachomsumbua.

Manara amesema kuwa alikula chakula chenye sumu, na ndio sababu iliyompelekea kulazwa na sio presha ya matokeo mabaya ya klabu yake kama inavyoandikwa mitandaoni.

“Siumwi pressure wala moyo kama inavyoandikwa mitandaoni..nahic nimepata food poisoning na niwashukuru Madaktari walionihudumia awali Shinyanga na Mwanza ..now nisharejea Dar teyari kwa vipimo zaidi…Insha’Allah kila kitu kitazidi kuwa salama,“ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Klabu ya Simba imekuwa na matokeo mabovu kwa msimu huu ambapo wiki iliyopita imepokea kichapo cha goli 1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad