Hakuna Siri Duniani Walioficha Watoto Wataumbuka Wote- Shilole

Hakuna Siri Duniani Walioficha Watoto Wataumbuka Wote- Shilole
BAADA ya sakata la mwanamama Rose Alphonce ‘Muna Love’ la kukana kwamba hana mtoto mwingine zaidi ya marehemu Patrick Peter kisha akaumbuka baada ya mtoto kuanikwa, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa mastaa wa kike wanaoficha watoto wataumbuka wote.

Akichonga na Za Motomoto News, Shilole alisema hakuna siri duniani na wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiwaficha watoto wao na kusema hawajawahi kuzaa au walizaa wakafa, ipo siku wataumbuka, pia wanatakiwa kutambua kuwa wanakosa riziki kwa sababu ya kuwaficha malaika hao wa Mungu.

“Hakuna siri duniani, ipo siku Mungu atawaumbua wote wanaodanganya kwamba hawana watoto au wamekufa, kuficha malaika hao wanakosa riziki ambazo wangepata kupitia wao, jamani wanawake wenzangu badilikeni, kuwa na mtoto au watoto siyo kashfa ni baraka maana wapo wanaotafuta wanakosa,” alisema Shilole.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad