Hakuna Wasanii Wenye Vipaji vya Kuzaliwa kwa Sasa Wengi Wanatengenezwa- Chemical

Hakuna Wasanii Wenye Vipaji vya Kuzaliwa kwa Sasa Wengi Wanatengenezwa- Chemical
Rapa wa kike wa bongo, Chemical 'Mwana wa Lubao' ameibuka na kudai kwamba kwa sasa hakuna wasanii wenye vipaji vya kuzaliwa, bali kumejaa watu wanaotengenezwa na kujifanya wanajua kuimba.

Chemical ameeleza hayo akiongea na eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV na kusema kwamba anawaonea huruma wasanii wachanga wanaoibukia ambao wanavipaji lakini hawana watu wa kuwa-support kwa kutoa pesa au kuwabeba ili nyimbo zao zirekodiwe studio na kuchezwa sehemu mbalimbali.

Hata hivyo Chemical ameendelea kusema kwamba "kuna watu ambao wanaharibu sanaa kwa sasa, unakuta mtu hajui kuimba anatumia hata wiki zima ku-record neno moja na kwa kuwa 'producer', analipwa haongei chochote tofauti na zamani ilikuwa msanii anaimba wimbo mzima mwanzo mwisho bila kuogopa chochote ila kwa sasa imekuwa ni changamoto kwa kweli".

Kwa upande mwingine, Chemical amesema hafurahishwi na hali ya sanaa inavyo kwenda kwa sasa kwa kuwa inazalisha watu wengi wabofu huku akiwaomba wadau wa muziki kujitokeza na kuweza kuwapa msaada wasanii wanaochipukia kwa lengo la kuviokoa vipaji vyao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad