Halima Mdee Aibua Sakata Jipya Bungeni

Halima Mbdee Aibua Sakata Jipya Bungeni
Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee, leo ameibua suala la ujenzi wa nyumba za kisasa 50,000 katika eneo la Kata ya Kawe lililookolewa kutoka mikononi mwa wawekezaji waliokuwa wakimiliki viwanda vya Tanganyika Packers.


Mdee ameuliza swali leo bungeni kwenda wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, lililohoji kwanini ujenzi wa mradi huo wa nyumba za kisasa ulioanza katika awamu ya nne umekwama katika awamu hii ya tano.

''Tulifanikiwa kuokoa eneo kutoka kwa wawekezaji uchwara wa Tanganyika Packers kwenye awamu ya nne na tukawakabidhi shirika la nyumba la taifa kwaajili ya kuliendeleza lakini hakuna kilichofanyika mpaka sasa'', amesisitiza Mdee.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amekiri kuwa eneo hilo halijaendelezwa kutokana na serikali ya awamu ya tano kubadili kipaumbele.

''Mradi huo na miradi mingine mingi ilisimama kwasababu serikali ilihamishia nguvu kwenye ujenzi wa miradi mipya makao makuu ya nchi Dodoma, lakini kwasasa miradi iliyosimama itaanza kufufuliwa kwasababu miradi ya Dodoma inaendelea vizuri'', amesema.

Miaka ya nyuma eneo la Tanganyika Packers kulikuwa na kiwanda cha serikali cha kusindika nyama kabla ya kubinafsishwa kwa mwekezaji ambaye alishindwa kukiendeleza ndipo serikali ikalichukua tena eneo hilo na kulikabidhi kwa NHC kwaajili ya ujenzi wa mji wa kisasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad