Hatimaye Darasa la Saba Wamaliza Mitihani

Darasa la saba wamaliza mitihani
Furaha ya kumaliza darasa la saba imetawala kwa wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho iliyoanza jana.

Baadhi ya wanafunzi wameonekana wakishangilia huku wengine wakipunga mikono kama ishara ya kuaga majengo ya shule. Somo la Maarifa ndilo lililokuwa la mwisho kufanyiwa mtihani.

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani (NACTE) wanafunzi 960,202 wamefanya mitihani hiyo huku kukiwa na ongezeko la 43,188 ikilinganishwa na mwaka jana.

Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya wanafunzi wamesema mitihani ilikuwa ya kawaida na wana uhakika wa kufaulu.

Faudhia John, Mwanafunzi wa shule ya msingi Hekima, Manispaa ya Ilala amesema  anatarajia kutimiza ndoto zake za kuwa daktari kwa sababu ana uhakika wa kufaulu.

"Maswali ni yaleyale ya kila siku, naamini nitafaulu vizuri kabisa kwa sababu nilijiandaa," amesema.

Mwanafunzi mwingine wa Shule ya Msingi BugurunI, Salum Ally alisema kwa sababu ufaulu wa wanafunzi hutokana na jitihada za kusoma, anaamini atafaulu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad