Hii Hapa Kauli ya Mrisho Gambo Baada ya CCM Kuibuka Mshindi Monduli

Hii Hapa Kauli ya Mrisho Gambo Baada ya CCM Kuibuka Mshindi Monduli
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Julius Kalanga amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo hilo kwa kupata ushindi wa kura 65,714 huku mpinzani wake Yonas  Laizer wa (CHADEMA)akipata kura 3,187.


Ushindi wa Julius Kalanga ulionekana kutabiriwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambae kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Alichapisha picha ikionesha kiongozi huyo akichuna ngozi ya mnyama na kuandika  ujumbe uliosomeka “Monduli kumenoga”  hali ambayo iliyoonekana ni maandalizi ya kusheherekea ushindi wa Julius Kalanga wa nafasi ya Ubunge.

Mapema leo asubuhi kupitia ukurasa huohuo wa Instagram Mrisho Gambo alichapisha picha ya wapambanaji wawili wa mchezo wa Judo mmoja akiwa na mwili mkubwa ambayo aliambatanisha na nembo ya CCM na mwingine mtu dhaifu ambayo pia aliambatanisha na nembo ya CHADEMA licha ya kutoandika chochote chapisho hilo liliashiria CHADEMA haiwezi kushindana na Chama hicho tawala.

Kupitia machapisho hayo baadhi ya wafuasi wanaomfatilia waliandika maoni mbalimbali wengine wakikipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi na wengine walionesha kutoridhishwa na ushindi Julius Kalanga kwa madai uchaguzi wa monduli ulikuwa na dosari.

Licha ya chama cha CHADEMA  kupitia mgombea wao Yonas Laizer kulalamika baadhi ya mambo kutokwenda sawa msimamizi wa Uchaguzi Stephen Ulaya amemtangaza Julius Kalanga kuwa mbunge mteule wa jimbo la Monduli.

Katika uchaguzi huo ilishuhudia wagombea wa vyama vingine akiwemo Wilfred Mlay wa ACT-Wazalendo akipata kura 144, Feruz Juma wa NRA kura 45, Simon Ngilisho wa Demokrasia Makini kura 35.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad