Hiki ndicho kilichomuokoa Mhandisi kivuko cha MV Nyerere


OIL imetajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizookoa maisha ya Mhandisi wa Kivuko cha MV Nyerere, Alphonce Charahani, aliyeokolewa akiwa hai baada ya kupita saa 48 tangu kivuko hicho kizame katika Ziwa Viktoria.

Wakizungumza baada ya kumuokoa mhandisi huyo, asubuhi ya leo tarehe 22 Septemba 2018, baadhi ya waokoaji walisema mbinu ya Mhandisi Charahani ya kujipaka oil mwilini, ilimsaidia kuzuia maji ya ziwa hilo kuingia kwenye vinyweleo vyake.

Kivuko hicho kilizama kwenye ajali iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018 wakati kikisafirisha abiria kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Kisiwa cha Ukara kwenye Ziwa Victoria.

Baada ya kuokolewa, Mhandisi Charahani alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Busya kilichopo kisiwani Ukerewe kwa matibabu zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad