Hili Hapa Jibu la Rich Mavoko Kwa Wanaomsema Amekonda "Unene ni Ugonjwa, Nashukuru Nimekonda’'

Hili Hapa Jibu la Rich Mavoko Kwa Wanaomsema Amekonda "Unene ni Ugonjwa, Nashukuru Nimekonda’'
Baada ya kuandamwa na maswali ya watu wengi mitandaoni wakihoji kuhusu  kuporomoka kwa afya yake, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko ameweka wazi juu ya afya yake kwa kusema kuwa ameteseka sana alivyokuwa kibonge kipindi cha nyuma.


Rich Mavoko amesema kuwa suala la kukonda amelipokea kwa mikono miwili kwani kuna wakati alikuwa mnene hadi alikuwa anashindwa kutembea umbali mrefu.

“Kwa miaka mitano hivi nimekuwa nikiteseka na kitambi, nakumbuka siku moja nilikutana na dada mmoja akaniambia yaani tumbo langu halifanani na umri wangu niliyokuwa nao, kiukweli niliumia kwa kauli ile.. Mwezi wa nane mwaka jana nikaanza mazoezi na Mungu akasaidia kitambi nikaondokana nacho, maana iliwahi kunitokea hali nikawa nashindwa kutembea umbali mrefu kutokana na pumzi zinajaa kwasababu ya kitambi,“amesema Rich Mavoko kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Kuhusu undani wa afya yake, Rich Mavoko amesema kuwa alishawahi kwenda Hospitali mara kadhaa kupima afya yake na alionekana yupo poa, ila ni unene ndio ulikuwa tatizo kwake.

“Nilijaribu kwenda hospitali nikaambiwa sina tatizo lolote ila nifanye mazoezi tu. Unene ni ugonjwa ndugu zangu, kwa hiyo nilivyopungua hivi mimi nashukuru na mnavyoniambia nimekonda nafurahi kwasababu nilishakata tamaa.“amemaliza Rich Mavoko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad