Hivi Ndivyo Chozi la Mkurugenzi Wilaya ya Serengeti Lilivyomuokoa Kutumbuliwa na JPM

Hivi Ndivyo Chozi la Mkurugenzi Wilaya ya Serengeti Lilivyomuokoa Kutumbuliwa na JPM
Mkurugenzi wilaya ya Serengeti bwana Juma Hamsini ameepuka rungu la mh; rais la kutumbuliwa baada ya mbunge wa wilaya hiyo kupitia chama cha Chadema bwana Marwa ryoba kumtaka mh;rais kuchukua uamuzi wa kumuondoa mkurugenzi huyo.



Bwana Marwa amedai kuwa mkurugenzi huyo ni mwizi sana ndio tatizo la wilaya hiyo kutoendelea mbunge huyo alisema:-“Mimi nakupenda Mh: rais lakini kwa mkurugenzi huyu tuna mkurugenzi mwizi, naomba niseme ameenda WMA akawalaghai wakampa milioni ishirini akaenda akakutana na aliyekuwa rasi wa mkoa akampa rasi wa mkoa milioni tatu akarudi milioni kumi na sana akaweka mfukoni eti anaenda kumugawia mkuu wa wilaya hakuwagawia akaweka mfukoni mpaka leo,Takukuru mkoa wanajua wilaya wanajua” mbunge huyo aliongeza ” Mh: rais sio hilo tu juzi kwenye kamati ya bunge mkurugenzi huyu wamefukuzwa na kamati ya bunge kutokana na fedha za miradi ya maendelea ambazo hazionekani kwa mujibu wa taarifa za CAG kwenye vikao pia haji,kwahiyo mh;rais mimi sio kwamba namsingizia ongea na vyombo vyako vya ulinzi na usalama watakwambia hafai ni mzigo”



Baada ya maelezo hayo ya mbunge huyo Mh; rais alichukua jukumu la kumuita mkurugenzi huyo mbele ili akajiele na mkurugenzi alianza kwa kusema:- ” Mh: rais mkoa wa Mara na wilaya zetu hizi za Serengeti na Tarime ni wilaya za ukinzani,binafsi nilikuwa sina ugonjwa wa moyo ila ugonjwa huu nimeupata wilaya ya Serengeti kwa sababu ya kuwatumikia wana Serengeti,kupitia mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya tulianzisha kauli mbiu inayosema jenga hospitali kupitia elfu moja na tulifanikiwa kuchanaga zaidi ya milioni 51 hospitali yetu iko hali nzuri na mimi mwenyewe kupitia mkuu wa mkoa tuliomba milioni 100 ilikuweza kukamisha awamu ya kwanza na Mh; rais umesikia kilio chetu umetutumia milioni 400. Mh: rais mikono yangu ni safi na salama wilaya hii ni changamoto sijaiba hata senti tano”



Baada ya mkurugenzi huyo kumpa maelezo Mh:rais yanayoeleweka rais aliamua kumuita mbunge na kumuuliza juu ya fedha ya wabunge zimefnya kazi gani huku wananchi wakimzomea na hapa rais aliamua kutoa maelezo kwamba ” Siwezi kumfukuza mtu kwa kumuonea ” huku mkurugenzi huyo akitokwa na mchozi ” na rais kusema tukiingiza mabo ya siasa hatutafanya kazi mimi nakupongeza kwa kufanya kazi nzuri utabaki hapa hapa na hela zote nilizotuma zimefanyiwa kazi endelea kufanya kazi utabaki hapa hapa” na rais kuongeza mbunge mzuri ni yule anayetengeneza ushirikiano mzuri na watu wake na hakuna mtu atakaye kufukuza na mimi ndio rais”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad