Hofu Yatanda Lindi Baaada ya Paka 12 Kuhudhuria Mazishi


Paka 12 washiriki mazishi ya bwana Salehe Matiko aliyeuawa kwa tuhuma za kuwa mshirikina

Inadaiwa kuwa Wanakijiji wa Chikalala walichoshwa na kile walichokiita ''MATESO YA MATIKO'' na kuamua kumvizia na kumshambulia hadi kumuua

Waombolezaji wakiwa njiani kuelekea makaburini, ghafla liliibuka kundi la Paka 12 lililoungana nao

Wakati wa kushusha maiti kwenye kaburi, Paka hao wanadaiwa kuinamisha vichwa chini huku Waombolezaji wakiwa na tahadhari ya lolote linaloweza kutokea

Aidha, baada ya mazishi, Paka hao waliendelea kubaki makaburini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad