Jaribio la Dawa ya HIV Lawapatia Matumaini Wanaoshiriki Tendo la Ngono Lisilo Salama

Jaribio la dawa ya HIV lawapatia matumaini wanaoshiriki tendo la ngono lisilo salama
Jaribio la dawa ya HIV ambayo inapunguza viwango vya maambukizi limekuwa likileta matumaini nchini Wales kulingana na takwimu mpya.

Vituo vya afya nchini Wales vilianza kutoa dawa hiyo ya Pre-Exposure Prophylaxis (Prep) mnamo mwezi Julai mwaka uliopita.

Katika mwaka wa kwanza wa majaribio, takriban watu 559 waliopo katika hatari ya maambukizi walitumia dawa hiyo ambayo imeelezewa kuleta matumaini ya kinga dhidi ya HIV.

Kati yao hakuna aliyepatikana na virusi vya HIV.

Wanajeshi wa Sudan Kusini wafungwa kwa ubakaji na mauaji
Kumekuwa na visa vya magonjwa ya zinaa miongoni mwa wale wanaoshiriki katika majaribio ya dawa hiyo, ambayo wanasayansi wamegundua inaweza kuwalinda watu waliopo katika hatari ya kupata maambukizi iwapo itatumiwa kila siku.

Phil alianza kutumia dawa hiyo baada ya kutoka katika uhusiano wa muda mrefu na kuona kwamba itakuwa njia nzuri ya kutahadhari.

'Inaondoa wasiwasi wa mtu kuambukizwa HIV'', aliambia BBC Radio Wales.

Inakupatia fursa ya kushiriki tendo la ngono bila wasiwasi.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad