JE, Wajua Takribani Nusu ya Watu Duniani Hukoroma Usingizini?


Kukoroma ni kutoa sauti kali kunakotokea ukiwa umelala. Sauti hiyo inatokea pale hewa unayopumua inapofanya tishu za nyuma ya koo kutetema na hutokea puani, mdomoni au sehemu zote mbili.

Takribani nusu ya watu duniani hukoroma katika sehemu fulani ya maisha yao. Kukoroma huwatokea zaidi wanaume kuliko wanawake na imeonekana kurithishwa katika familia.

Kulalia mgongo, au magonjwa ya mafua na kikohozi huweza kusababisha kukoroma. Pia huweza kusababishwa na misuli ya koo kulegea kutokana na matumizi ya pombe. Hali ya kukoroma hutokea zaidi kwa watu wenye umri mkubwa.

Ili kuepuka kukoroma inashauriwa kubadili mtindo wa kulala kwa kuacha kulala chali, kutumia mto unaoweza kuegemeza mwili mzima, kuacha kunywa pombe hususan kabla ya muda wa kulala, kufanya mazoezi ya kupunguza uzito na kuoga ama kunywa maji ya moto ili kuzibua njia ya pua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad