Je Wajua Yondani Alivyoondoka Simba Pengo Lake Liliigharimu Simba Kwa Muda Mrefu?


Inawezekana mchezaji mmoja akiondoka kwenye timu akaharibu mfumo mzima wa uchezaji katika timu husika? Jibu ni NDIYO.

Kiungo wa zamani wa Simba Amri Kiemba amesema hii kitu ilishawahi kuwakuta Simba baada ya beki wa kati Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga.

"Kipindi tunacheza Simba aliondoka Yondani, ni kipindi ambacho Simba ilinunua mabeki wengi na kuwaacha, walikuja wacongo na kina Keita yote katika kutafuta kuziba pengo la Yondani"-Amri Kiemba.

"Kwa wakati huo safu ya ulinzi ilitengenezwa kupitia Yondani baada ya Owino kuondoka. Kwa hiyo Yondani akawa muhimili wa ulinzi mabeki wote walikuwa wanacheza kwa kutegemea Yondani anachezaje."

"Alipoondoka Simba ilikuwa inajaribu kwa njia zote inapataje mtu kama Yondani, ndio kipindi ambacho ilipoteza pesa nyingi kununua walinzi  kwa wakati huo."


Timu gani nyingine imewahi kuhangaika baada ya kuondokewa na mchezaji wake muhimu?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad