Jenerali Mabeyo Amsifu Magufuli Sakata la Kuzama MV Nyerere..Alikuwa Halali


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, amesema uongozi mahiri wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli umewezesha kasi ya uokoaji na kuibua kivuko cha MV. Nyerere kufanyika kwa mafanikio makubwa.


Jenerali Mabeyo ameyasema hayo katika misa maalumu ya kuwaombea marehemu waliokufa katika ajali ya ya kivuko cha MV Nyerere, iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yuda Thadei, iliyopo Ilumia, Magu Mkoani Mwanza.

Mabeyo amesema kazi ya kubwa kuokoa kivuko kilichokuwa kimezama imesimamiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania ikishirikiana na vyombo vengine vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Ukerewe.

"Kama ambavyo hilivyo Jeshi likipewa maelekezo au amri linatekeleza kwa uweredi, na sisi tunapojipangia kazi huwa tunajiwekea na malengo,baada ya siku tatu hadi nne tukawa tumekitoa kivuko majini na watanzania wameshuhudia,daima tuto tayari kutekeleza majukumu yetu....

Tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa umahiri wake amekuwa akitusapoti muda wote, alikuwa halali amekuwa akitupigia simu kujua maendeleo ya huku nasisi hatukusita kumpatia yaliyokuwa yanajiri", amesema Jenerali Mabeyo.

Zoezi hilo la kukinasua kivuko hicho kilichokuwa kimezama katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018 tayari limekamilika na kwa sasa serikali inaendelea na uchunguzi juu ya ajali hiyo iliyoua watu 228, huku tayari Rais Magufuli ameamuru kukarabatiwa kwa kivuko kingine kitakacho beba watu zaidi ya 300.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad