Jinsi ya Kuzuia Mtoto Mwenye Tatizo la Kukojoa Kitandani Asijikojolee

Mtoto kukojoa kitandani inazuilika na mara nyingine sio hata ugonjwa ni malezi tu. Ingawa mara nyingi huwa ni ugonjwa na huitaji ushauri wa daktari na hutibika kabisa.

Hapa tutaangalia njia za kuzuia mtoto kukojoa kitandani kwa wale ambao hawana matatizo ya kitabibu;


Njia ya kwanza ni kuthibiti unywaji wa vimiminika masaa machache kabla ya kulala au wakati wa usiku. Hakikisha anaenda kukojoa kabla hajaenda kulala na ulisimamie hili.
Njia ya pili ni kumuamsha wakati wa siku kwa ajili ya haja ndogo ili kuzuia kukojoa kitandani, mara kwa mara. Weka hata kengele ya kwenye saa ikukumbushe kila baada ya masaa mawili au matatu. Kesho yake akikojoa tena rudisha yale masaa na umwamshe baada ya lisaa limoja na nusu kila siku.
Njia nyingine ni Asali mbichi, mpe mtoto kijiko kidogo cha asali mbichi kabla ya kulala kila siku, mpaka atakapo pona. Unaweza kumpakia kwenye mkate wakati wa chai asubui.
Mdalasini pia ni dawa nzuri sana kwa watoto wenye matatizo ya kukojoa kitandani, huufanya mwili wa mtoto kupata joto ambalo huzuia kukojoa kitandani. Chukua unga wa mdalasini kijiko kidogo kisha changanya na asali halafu paka kwenye mkate au uchanganye kwenye maziwa fresh.


Masaji, hii pia ni dawa nzuri kwa kuzuia kukojoa kitandani, tumia mafuta ya zeituni (olive oil) yachemshe kidogo yapate uvuvugu alafu mfanyie massage mtoto chini ya tumbo. Fanya ivo mara kadha,  taratibu taratibu.
Usimpige mtoto kwa sababu ya kukojoa kitandani wala kumfokea bali mlee kwa upendo na uwe unampa zawadi kila mara asipokojoa kumpa moyo. Pia usiku uhakikishe njia ya kwenda chooni ina mwanga wa kutosha kwa kua watoto huogopa giza pamoja na hilo msindikize mpaka atakapokua na uwezo wa kwenda mwenyewe. Fanya mambo kwa upendo nae atakua anaelewa na kuacha kukojoa kitandani. Kama hizo njia zote zikishindikana mpeleke kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad