Jokate Apata Shavu Lingine, Ateuliwa na SZIFF


MSIMU wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es salaam na kumtangaza, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kuwa Mlezi wa tuzo hizo.

Katika uzinduzi huo, DC Jokate Mwegelo alitangazwa kuwa mlezi wa tuzo za SZIFF kwa msimu wa pili na kuahidi kuhamasisha vijana kujikita zaidi katika ubunifu wa sanaa ya uigizaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na Mlezi wa Tuzo za SZIFF Jokate Mwegelo amesema kuwa anafurahi sana kupewa nafasi ya kuwa mlezi wa tuzo hizo kwani hata yeye alikuwa  katika tasnia ya filamu akiwa amecheza filamu mbalimbali.

Amesema kuwa, tuzo hizi zimeleta chachu ya wasanii kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa na kuhamasisha zaidi vijana kufanya kazi za sanaa kwani  inawapatia kipato wasanii wengi sana ila wanahitaji mtu wa kuwasaidia kuinua na tuzo hizi za SZIFF zimekuwa na mchango mkubwa sana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad