Jokate Atoa ya Moyoni Kuhusu Miss Tanzania

Jokate Atoa ya Moyoni Kuhusu Miss Tanzania
Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefunguka na kumpongeza Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune kwa kuweza kunyakua taji hilo na kumpa baraka zake nyingi katika kupeperusha bendera kuelekea michuano ya kumtafuta mrembo wa dunia.
.

Jokate ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wa Instagram asubuhi ya leo Septemba 11, 2018, ambapo alianza kuelezea kwa ufupi juu ya safari yake katika ulimbwende hadi kufikia hatua ya kujikita katika masuala ya siasa huku akiwasisitiza mabinti kutokubali kukatishwa tamaa katika kuzipigania ndoto zao.

"Hongera sana Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth Makune kwa kushinda taji hilo nenda ukapeperushe bendera ya Tanzania, una baraka zote kutoka kwetu. Kwa washiriki wote wa Miss Tanzania wa mwaka huu hongereni kwa kuweza kushiriki na kuyafanikisha mashindano haya na hiyo ni fursa pekee kwenu, muitumie kwa manufaa yenu pamoja na taifa", ameandika Jokate.

Mbali na hilo, Mhe. Jokate amempongeza Basila Mwanukuzi kwa kuweza kurejesha heshima ya Miss Tanzania ambayo ili kuwa imepotea kwa miaka kadhaa kwa jamii pamoja na washiriki wenyewe.

"Kupitia wewe, wasichana watanufaika katika kutimiza ndoto zao kama neno linalovyosema 'when something is important enough, you do it even if the odds are not in your favor'. Hongera sana dada yangu maana umefanikiwa kufanya 'show' kubwa hata bila ya kutegemea wadhamini na rasilimali za kutosha lakini hukukatishwa tamaa na hatimaye umeweza. 'Looking forward to what the future holds for Miss Tanzania under your leadership and thank you for making that contribution for education in Kisarawe", amesisitiza Jokate.

Jokate Mwegelo licha ya kuwa Mkuu wa Wilaya, alishawahi kushiriki kulisaka taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kuibukia mshindi wa pili, Lisa Jensen kuwa mshindi wa tatu huku Wema Sepetu akitajwa kuwa Miss Tanzania kwa mwaka huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad