Imekuwa ikizoeleka kuwa wasanii wengi wenye majina huwa inakuwa ngumu sana kuwa karibu na kufanya mambo kwa pamoja,kuna muda inakuwa kama kuna pepo linawapitia wasanii hawa wakubwa tena hasa wa kike na kujikuta kuwa hawana mahusiano mazuri.
Hii imekuwa ikitokea asio tu kwa Tanzania lakini pia haa nchi za jirani wasanii wengi wa kike wamekuwa hawaelewani sana na hata kukutana yao inakuwa katika yale matukio tu yanayoweza kuwalazimu kukutana.
Lakini hii ni tofauti kwa mwanadada Jokate na Nandy ambao wanasemekana kuwa ni marafiki lakini pia ni watu wanaoshauriana sana ktika kazi na maisha.
Akiongea na waandishi wa habari, Nandy anathibitisha hayo na kusema kuwa ” DC JOKATE NI ZAIDI YA RAFIKI KWANGU, NI MSHAURI WANGU MKUBWA ANAUUPENDA SANA MUZIKI WANGU NA ANANIPENDA MIMI PIA”